UGANDA-MUSEVENI

Museveni amteua mkewe kwenye wadhifa wa Waziri wa Elimu

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. RFI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, aliyechaguliwa mwezi Februari kwa muhula wa tano baada ya uchaguzi wenye utata, amemteua mke wake kuwa Waziri wa Elimu na Michezo chini ya mfumo wa uundwaji mpya wa serikali yake, Ofisi ya rais imearifu Jumanne hii.

Matangazo ya kibiashara

Janet Museveni, mwenye umri wa miaka 67, aliyekuwa Mbunge, hajulikanikatika uwanja wa siasa nchini Uganda. Tangu 2011 alikua kama Waziri msimamizi wa Karamoja, mkoa changa wa kaskazini mashariki mwa Uganda.

Uteuzi wake umetangazwa katika taarifa kutoka Ofisi ya rais ambayo imeeleza mabadiliko madogo katika serikali, yenye mawaziri na makatibu dola 80.

"Uteuzi huu mpya ulikua unasubiriwa, Museveni ameweka ajenda ya familia yake katika siasa nchini Uganda", ameshtumu Ken Lukyamuzi, Mbunge wa zamani kutoka kambi ya upinzani aliye kuwa akishiriki vikao vya Bunge pamoja na Janet Museveni. "Hivi karibuni alidai kumteua mwanae kwenye cheo cha juu jeshini (jenerali), na sasa mke wake kwa mara nyingine tena kauteuliwa waziri," Ken Lukyamuzi ameliambioa shirika la habari la AFP.

Mei 25, Muhoozi Kainerugaba, mwanae Museveni, alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa vikosi Maalum. Kainerugaba alikanusha kutaka kumrithi baba yake kama mkuu wa nchi huku upinzani ukisema kuwa Museveni alikuwa akimuandaa kuchukua nafasi yake.

uteuzi mwingine muhimu, Simon Lokodo, mwanasiasa mashuhuri, ameteuliwa kuwa Katibu dola anayehusika na masuala ya Maadili na Uadilifu, katika nchi ambapo ushoga unahukumiwa kwa adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Museveni, mwenye umri wa miaka 71 ambaye yuko madarakani kwa 30 sasa, alichaguliwa mwezi Februari kwa muhula wa tano kwa 61% ya kura baada ya uchaguzi wenye utata ambao upinzani umeendelea kupinga matokeo.