BURUNDI-USALAMA

Mwandishi wa Bonesha Fm achiliwa huru

Bujumbura, Februari 3, 2016. Burundi, mzunguko wa vurugu na ukandamizaji vinandelea kushuhudiwa kwa mwaka mmoja sasa.
Bujumbura, Februari 3, 2016. Burundi, mzunguko wa vurugu na ukandamizaji vinandelea kushuhudiwa kwa mwaka mmoja sasa. © REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana

Mwandishi wa habari wa Burundi aliyekamatwa Jumapili na polisi katika mkoa wa Cibitoke (kaskazini magharibi) na kukabidhiwa kwa Idara ya Ujasusi ameachiliwa huru Jumanne hii, vyanzo vya polisi na mashahidi wamebaini.

Matangazo ya kibiashara

"Mwandishi Egide Ndayisenga yuko huru, ameachiliwa na mwendesha mashtaka katika mkoa wa Cibitoke dakika chache zilizopita," chanzo cha polisi kimeliambia shirika la habari la AFP.

Taarifa hii imethibitishwa na marafiki wa mwandishi huyo, ambao wamemuona na kuzunumza naye. "Anaendelea vizuri licha ya ya kupitia katika mazingira ambayo hakuzowea," mmoja wao wa marafiki zake amesema.

Mwandishi huyo wa kituo binafsi cha Bonesha FM , menye umri wa miaka 28, alikamatwa Jumapili asubuhi wakati alikuwa katika mkoa wa Cibitoke, kaskazini magharibi mwa Burundi. Egide Ndayisenga alikua alitembelea marafiki zake tangu Jumamosi, katika mkoa wa Cibitoke.

Awali alizuiliwa katika majengo ya Idara ya Ujasusi, kabla ya kupelekwa Jumatatu katika kituo cha polisi kwa amri ya mwendesha mashitaka mkoani Cibitoke.

Kwa mujibu wa chanzo kingine cha polisi, Egide Ndayisenga alioulizwa kuhusu uhusiano na "vituo vya redio za upinzani zinazorusha matangazo yao kutoka Rwanda" na kuhusu safari anazofanya mara kwa mara katika nchi hiyo ambapo mahusiano kati ya nchi hiyo na utawala wa Bujumbura yako katika hali ya sintofahamu. Egide Ndayisenga alikana shutma hizo, chanzo hicho kilisema.