EAC-BAJETI

Mawaziri wa Fedha kutoka EAC wawasilisha bajeti za nchi zao

John Pombe Magufuli, mmoja wa maris wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mwaka huu.
John Pombe Magufuli, mmoja wa maris wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mwaka huu. AFP Photo/Daniel Hayduk

Mawaziri wa Fedha, uchumi na mipango kutoka nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki, hapo jana jioni waliwasilisha bajeti za nchi zao kwa wakati mmoja, bajeti ambazo baadhi zimepongezwa na baadhi zimekosolewa.

Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Tanzania ilitangaza kiasi cha Trilioni 29 kutumika kwenye bajeti yake, huku nchi ya Rwanda ikitangaza kiasi cha fedha ya Rwanda bilioni 949, Kenya ikitangaza kiasi cha Trilioni 2.3 na Uganda ikitangaza kiasi cha shilingi za Uganda trilioni 26.

Kwenye bajeti hizo baadhi ya kodi zisizo za lazima zimeondolewa na maeneo mengine kuongezewa kodi, huku vitu kama sigara na vimiminika vingine vikiongezewa kodi hatua inayomaanisha kuwa vitapanda bei kwa nchi zote.

Profesa Ibrahim Lipumba, mtaalamu na gwiji wa uchumi wa dunia, amesema Tanzania imejitahidi kutenga fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo, lakini amebaini kwamba changamoto bado ni kubwa, licha ya nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki bado zinategemea misaada kwa kiasi kikubwa kutoka nje.