KENYA-CORD-SIASA

Upinzani wa Kenya waitwika lawama serikali

Kiongozi mkuu wa upinzani Kenya, Raila Odinga wakati wa sherehe ya maadhimisho ya Madaraka Day,Juni 1, 2016.
Kiongozi mkuu wa upinzani Kenya, Raila Odinga wakati wa sherehe ya maadhimisho ya Madaraka Day,Juni 1, 2016. REUTERS/Goran Tomasevic

Viongozi wa upinzani nchini Kenya wakiongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, wamezuiliwa na polisi kuonana na wanasiasa sita wa upinzani wanaozuiliwa katika kituo cha polisi cha Pangani jijini Nairobi kwa madai ya kutoa matamshi ya uchochezi.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wameshtumu hatua ya serikali kuwazuia wanasiasa hao kwa siku ya tatu leo bila ya kuwafungulia mashtaka na kukataa kuonana na wapendwa wao.

Inaripotiwa kuwa wanasiasa hao wamekataa kula chakula cha rumande na wapendwa wao waliowapelea chakuka na nguo za kubadilisha walizuiliwa.

Upinzani sasa unataka wanasiasa wote kuachiliwa huru kwa saa 24 zijazo la sivyo watachukua hatua.

Mahakama siku ya Jumanne wiki hii iliamuru wanasiasa hao kuzuiliwa hadi Ijumaa hii ili kuruhusu polisi kukamilisha uchunguzi dhidi yao.