AL- SHABAB

Al Shabab yawauwa polisi watano nchini Kenya

Magaidi wa Al Shabab nchini Somalia
Magaidi wa Al Shabab nchini Somalia Reuters

Kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka nchini Somalia, limewauawa maafisa watano wa polisi wa Kenya katika Kaunti ya Mandera Kaskazini mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Gavana wa Kaunti hiyo Ali Roba amesema maafisa hao walishambuliwa baada ya kuviziwa wakiwa ndani ya gari lao katika eneo la Dimu.

Ripoti zinasema afisa mwingine wa polisi ametoweka baada ya shambulizi hilo lililotokea wakati maafisa hao wakisindikiza basi la abiria kwenda mjini Mandera.

Gavana Roba, amelaani mauaji hayo ya polisi na kusema wakaazi wa Kaunti hiyo walikuwa na habari za uwezekano wa kutokea kwa shambulizi hilo na kuzitoa kwa maafisa wa usalama lakini zilipuuzwa.

“Inasikitisha kuwa, raia walikuwa na taarifa hizi wakazisambaza,” alisema.

Hii ni mara ya tatu kwa basi la abiria aina ya Makkah kushambuliwa na kundi hilo, likiwa njiani kutoka jijini Nairobi kwenda mjini Mandera.

Mwaka 2014, basi hilo lilishambuliwa tena na kusababisha vifo vya wakiristo 28.

Ripoti za Kiinteljensia mwishoni mwa mwezi uliopita, zilieleza kuwa washukiwa 45 wa Al Shabab waliingia nchini Kenya tarehe 29 kutokea nchini Somalia.

Tangu mwaka 2011, jeshi la Kenya lilipoingia Somalia, nchi hiyo imekuwa ikishambuliwa na magaidi wa Al Shabab, mashambulizi ambayo hata hivyo yamepungua katika siku za hivi karibuni.