Uganda

Kesi dhidi ya mauaji ya viongozi wa dini ya Kiislamu nchini Uganda yaanza

Polisi nchini Uganda wakiwa nje ya Mahakama jijini Kampala
Polisi nchini Uganda wakiwa nje ya Mahakama jijini Kampala Daily Moniter

Usalama umeimarishwa katika Mahakama Kuu jijini Kampala nchini Uganda, wakati huu kesi ya mauaji dhidi ya washukiwa 32 ikiendelea.

Matangazo ya kibiashara

Washukiwa hao wanaongozwa na kiongozi wao Yunus Kamoga kutoka kundi linalojiita la Tabliq.

Watu hao wanashukiwa kutekeleza mauaji ya viongozi kadhaa wa dini ya Kiislamu jijini Kampala mwaka uliopita.

Miongoni mwa viongozi waliopoteza maisha ni pamoja na Sheikh Mustafa aliyeuawa mwaka jana katika eneo la Bahiga Bwebajja, katika barabara ya Entebbe.

Wengine ni pamoja na Sheikh Abdulkadir Muwaya aliyeuawa katika Wilaya ya Mayuge na Sheikh Hassan Kirya aliyepigwa risasi katika Wilaya ya Wakiso.

Washukiwa hao walifika Mahakama saa mbili asubuhi chini ya ulinzi mkali kutoka katika Gereza la Luzira wanakozuiliwa.

Mauaji ya viongozi hao wa dini ya Kiislamu yalizua hali ya wasiwasi nchini Uganda na kuyahusisha na mashambulizi ya kigaidi ya kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia.