Habari RFI-Ki

Wabunge wa Upinzani UKAWA wasusia vikao,wakilenga kutetea demokrasia

Sauti 09:33
Wabunge wa vyama vya upinzani walipokuwa wakianza kutoka Bungeni, Jumatatu, June 20, 2016.
Wabunge wa vyama vya upinzani walipokuwa wakianza kutoka Bungeni, Jumatatu, June 20, 2016. RFI

Karibu katika makala ya habari rafiki leo tunazungumzia hatua ya wabunge wanaounda muungano wa upinzani UKAWA nchini Tanzania kuendelea kususia vikao vya bunge na kuzua mjadala wa kisiasa wakati huu wakijiapiza kuendelea kutetea demokrasia.Spika wa Bunge amesema ni haki yao kugoma lakini hakutakuwa na malipo kwa mbunge asiyeshiriki vikao.Una maoni gani msikilizaji?Kuna haja ya kuwepo maridhiano kati ya pande hizo mbili?hatima yake ni nini?