UGANDA

Polisi nchini Uganda waongoza kwa ufisadi

Polisi wa Uganda
Polisi wa Uganda Observer

Ripoti ya idara ya ukaguzi wa fedha za umma nchini Uganda inaonesha kuwa polisi nchini humo wanaendelea kuongoza katika upokeaji wa rushwa.

Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi uliofanyika mwaka uliopita umebaini kuwa, asilimia 75 ya Waganda waliohojiwa, walikiri kutoa kutoa fedha au kitu kingine kwa polisi ili kuhudumiwa.

Mwezi Desemba mwaka jana, shirika lingine la Afrobarometer lilitoa ripoti yake na pia kubaini polisi kuendelea kuongoza katika sakata hilo na kuishauri serikali kuifanyia mabadiliko, idara hiyo.

Inspekta Mkuu wa polisi nchini Uganda Kale Kaihura
Inspekta Mkuu wa polisi nchini Uganda Kale Kaihura http://allafrica.com/

Inspekta Mkuu wa Polisi Kale Kaihura ametupilia mbali ripoti hiyo na kusema, ripoti hizi zimekuwa zikitolewa kila mwaka na hazina jambo lolote jipya na kusisitiza kuwa idara yake imeweka mikakati ya kukabiliana ipasavyo na ufisadi.