KENYA

Wanasiasa nchini Kenya kuanza mazungumzo kuhusu tume ya Uchaguzi

Mfuasi wa upinzani akiandamana jijini Nairobi
Mfuasi wa upinzani akiandamana jijini Nairobi REUTERS/Thomas Mukoya

Mazungumzo ya kisiasa kuhusu marekebisho ya Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka ujao, yanatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya serikali na upinzani kukubaliana kuunda kamati maalum ya wajumbe 14 kila upande ukitoa wajumbe 7 kujadili suala hilo tata.

Mazungumzo haya yanakuja baada ya msururu wa maandamano ya upinzani kushinikiza kujiuzulu kwa Makamishena wa Tume ya Uchaguzi, kwa madai kuwa hawawezi kusimamia uchaguzi ujao kwa sababu si huru lakini pia ni wafisadi, tuhma ambazo Makamishena hao wameendelea kukanusha.

Waandamanaji nchini Kenya
Waandamanaji nchini Kenya REUTERS/Goran Tomasevic

Vyombo vya Habari nchini Kenya vinaripoti kuwa baada ya mwafaka kupatikana, mswada maalum utawasilishwa bungeni ili wabunge waunge mkono mapendekezo yatakayokuwa yemekubaliwa katika kamati hiyo.

Viongozi wa dini na Mabalozi mbalimbali hasa Balozi wa Marekani nchini humo Robert Godec, wamekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanasiasa wa upinzani na serikali wanazungumza na kupata mwafaka.

 Uchaguzi Mkuu nchini Kenya untarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka ujao.