Uganda

Watu zaidi ya 20 wapoteza maisha katika ajali jijini Kampala

Takribani watu 20 wamepoteza maisha leo Jumapili katika ajali ya barabarani kwenye barabara kuu nje ya mji mkuu wa Uganda, Kampala na wengine kadhaa wamejeruhiwa,wengine wako katika hali mbaya polisi imesema.

Muonekano wa jiji la Kampala nchini Uganda
Muonekano wa jiji la Kampala nchini Uganda RFI/Victor Abuso
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa polisi Phillip Mukasa ameithibitishia AFP taarifa za ajali hiyo na kuongeza kuwa majeruhi wamepelekwa hospitalini kutoka na majeraha makubwa waliyopata.

Magari matano yamehusika katika ajali hiyo katika barabara kuu ya Kampala-Masaka wakati gari binafsi lilipokuwa likijaribu kuyapita magari mengi katika njia yenye magari mengi umbali wa kilometa 150 Kusini Magharibi mwa mji mkuu Kampala.