RWANDA-ISRAEL

Benjamin Netanyahu ziarani Rwanda

Baada ya Uganda na Kenya, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaendelea na ziara yake katika ukanda wa kusini mwa Sahara. Leo Jumatano anaifanya hatua ya tatu ya ziara yake nchini Rwanda.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, akiwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda, Julai 4, 2016, siku mbili kabla ya ziara yake nchini Rwanda.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, akiwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda, Julai 4, 2016, siku mbili kabla ya ziara yake nchini Rwanda. REUTERS/Presidential Press Unit/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ni maalum ambayo imejaa na hisia mbalimbali. Waziri Mkuu wa Israel atazuru eneo la Gisozi mjini Kigali, kulikojengwa Mnara wa makumbusho ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994. Rwanda na Israel zina mahusiano mazuri, ukaribu unaoelezwa kwa historia ya kutisha inayofanana kwa nchi hizi mbili.

"Tunaiujenga nchi kwa ulimwengu wa kileo kwa majivu ya mauaji ya kimbari. Na tuna mfano wa kuiga, " balozi wa Rwanda nchini Israel ameviambia hivi karibuni vyombo vya habari.

Uhusiano kati ya nchi hizi mbili uliimarika mwaka 2013 wakati wa ziara ya Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mji wa Jerusalem. "Mauaji ya kimbari ni suala umuhimu kisaikolojia katika uhusiano huu," amesema Ely Karmon, mtaalam dhidi ya ugaidi kutoka Israel.

Kwa mujibu wa Phil Clark, mtaalam wa masuala ya Rwanda katika Chuo Kikuu cha SOAS, ziara ya Waziri Mkuu wa Israel "ina maana kubwa kwa nchi zote mbili." Kwa upande wa Rwanda, Israel ni chaguo mbadala wakati ambapo mahusiano yake si mazuri na Washington au hata London.

Israel inawezainaweza kuwa na matumaini kwa baadhi ya misaada kutoka Rwanda kimataifa. Kwa hiyo kama Rwanda inapendelea ufumbuzi katika mgogoro wa Israel na Palestina, mwaka 2014 wakati nchi hiyo ilikua mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ilijizuia kupigia kura azimio lililolenga mwisho wa uvamizi wa maeneo ya Palestina.

Baada ya Uganda na Kenya, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaendelea na ziara yake katika ukanda wa kusini mwa Sahara. Leo Jumatatno anaifanya hatua ya tatu ya ziara yake nchini Rwanda. Hatua hii ni maalum ambayo imejaa na hisia mbalimbali. Waziri Mkuu wa Israel atazuru eneo la Gisozi mjini Kigali, kulikojengwa Mnara wa makumbusho ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994. Rwanda na Israel zina mahusiano mazuri, ukaribu unaoelezwa kwa historia ya kutisha inayofanana kwa nchi hizi mbili.

"Tunaiujenga nchi kwa ulimwengu wa kileo kwa majivu ya mauaji ya kimbari. Na tuna mfano wa kuiga, " balozi wa Rwanda nchini Israel aliviambia hivi karibuni vyombo vya habari.