BURUNDI

Mazungumzo ya amani kuhusu Burundi, yasogezwa mbele hadi Julai 12

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, akikumbatiana na rais wa Afrika Kusini, Jackob Zuma
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, akikumbatiana na rais wa Afrika Kusini, Jackob Zuma Reuters/Evrard Ngendakumana

Mazungumzo ya amani kuhusu nchi ya Burundi, yaliyozinduliwa mwezi May mwaka huu baada ya miezi kadhaa ya mvutano, yameahirishwa kutoka siku ya Jumamosi hadi Jumanne ya wiki ijayo nchini Tanzania, imesema taarifa ya mratibu wa mazungumzo na wanadiplomasia wanaoshiriki mazungumzo. 

Matangazo ya kibiashara

"Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, mazungumzo kuhusu mzozo wa Burundi, yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kuanzia Julai 9 hadi 12 jijini Arusha, yameahirishwa, amesema Makocha Tembele, msaidizi wa rais Bejamin Mkapa anayeratibu mazungumzo hayo.

Wanasiasa kadhaa wa Burundi wamethibitisha kupokea ujumbe ukiwataarifu kuwa sasa mazungumzo yatafanyika Jumanne ya wiki ijayo", taarifa ambayo imethibitishw apia na mwanadiplomasia ya Umoja wa Ulaya ambaye hakupenda jina lake kuwekwa wazi.

Licha ya shinikizo na vitisho vya kuwekewa vikwazo kutoka Juumuiya ya kimataifa, utawala nchini Burundi umekataa katakata kukaa meza moja na viongozi wakuu wa upinzani, ikiwatuhumu wapinazani hao kushiriki njama za kutaka kuipindua Serikali mwezi Mei mwaka jana.

Nchi ya Burundi ilitumbukia kwenye machafuko ya kisiasa, wakati rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu mwezi April mwaka jana, kabla ya kuchaguliwa tena mwezi Julai.

Mpaka sasa machafuko ya Burundi, yameripotiwa kusababisha vifo vya watu 500 na tume ya umoja wa Mataifa inayohusika na wakimbizi UNHCR, inakadiria kuwa watu zaidi ya laki 3 na elfu 70 raia wa Burundi wamekimbia nchi yao.