TANZANIA-INDIA

Waziri mkuu wa India awasili Tanzania

Waziri mkuu wa India Narendra Modi
Waziri mkuu wa India Narendra Modi 路透社

Waziri mkuu wa India Narendra Modi amewasili nchini Tanzania jana usiku kwa ziara ya siku moja ,kama sehemu ya ziara yake ya siku tano barani Afrika kwa lengo la kukuza uhusiano wa nchi hiyo na bara la Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Modi amewasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na kupokelewa na waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na waziri wa mambo ya kigeni, ushirikiano wa kimataifa, Afrika mashariki na kikanda Balozi Augustino Mahiga.

Ziara ya Modi inalenga kukuza ushirikiano baina ya Tanzania na India katika sekta mbalimbali kama vile, kilimo,elimu, bishara, viwanda, maji na nyingine kwa lengo la kukuza uchumi.

Baadaye hii leo Modi atakuwa na mazungumzo rasmi na mwenyeji wake rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli

Katika ziara hiyo waziri mkuu Modi amefuatana na wafanyabiashara na wawekezaji wapatao hamsini kutoka katika sekta mbalimbali nchini India.