BURUNDI-BENJAMIN MKAPA-MAZUNGUMZO

Serikali ya Burundi yasusia uzinduzi wa mazungumzo Arusha

Wanajeshi na askari polisi wakipiga doria katika mtaa mmoja wa Bujumbura, Februari 3, 2016.
Wanajeshi na askari polisi wakipiga doria katika mtaa mmoja wa Bujumbura, Februari 3, 2016. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimama

Mazungumzo juu ya mustakabali wa Burundi yaliyokua yatanatazamiwa kuanza Jumanne hii Julai 12 katika mji wa Arusha, nchini Tanzania yamegubikwa na hali ya sintofahamu, baada ya wajumbe wa Serikali na wale wa chama tawala CNDD-FDD kususia uzinduzi wa mazungumzo hayo mapema mchana.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yanafanyika ili kujaribu kuindoa nchi hiyo katika mgogoro unaoendelea. Kwa kikao hiki cha pili, Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa anaukutanisha utawala wa Bujumbura, upinzani uliolibaki Burundi, na baadhi ya wanaharakati wa vyama vya kiraia.

Hali hiyo imeibuka baada ya baadhi ya wanasiasa kutoka kambi ya upinzani walio uhamishoni na wanaharakati wa vyama vya kiraia walioanzisha maandamano dhidi ya muhulawa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza kupewa mwaliko wa kushiriki mazungumzo hayo. Watu hao ni pamoja na Jean Minani, kiongozi wa muungano wa wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni (CNARED) na wanaharakati watatu, ambao ni miongoni mwa waanzilishi wa maandamano dhidi ya muhula watatu wa Rais Pierre Nkurunziza, ikiwa ni pamoja na Armel Niyongere na Pacifique Nininahazwe.

Wajumbe wa Serikali ya Bujumbura wanasema kuwa watu hao walishiriki katika jaribio la mapinduzi yaliyotibuliwa Mei 13 na 14 mwaka 2015.

Mshauri mkuu wa Rais Nkurunziza katika masuala ya mawasiliano, Willy Nyamitwe, amesema Jean Minani, Armel Niyongere na Pacifique Nininahazwe wanatafutwa na vyombo vya sheria vya Burundi, kwa hiyo hawawezi kualikwa katika mazungumzo ya Arusha.

CNARED bado haijatambuliwa ...

Serikali ya Burundi imeendelea kusema kuwa mashauriano tayari yameanza nchini Burundi baina ya Warundi. Tume iliyoteuliwa na utawala wa Bujumbura kwa minajili ya kuendesha maungumzo baina ya wadau walio ndani ya nchinii inaendelea na mazungumzo tangu miezi kadhaa, na kuweza kufikia katika uundwaji wa Katiba mpya.

Serikali inasema, wale utawala wa Bujumbura unawachukulia kama "magaidi" wametengwa katika mashauriano hayo. Serikali, hapo, inalenga muungano wa wanasiasa wa upinzani (CNARED). Hakuna mazungumzo yanayowezekana: serikali ya Bujumbura inakataa katu katu kukaa kwenye meza moja na CNARED.

Mwishoni mwa juma hili, msuluhishi katika mgogoro wa Burundi, Benjamin Mkapa atawasilisha mpangilio wa mazungumzo kwa Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, nje ya mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Kigali.