Jeshi la Uganda laingia Sudan Kusini

Hali ya usalama bado ni ya wasiwasi nchini Sudan Kusini licha ya hali ya utulivu kurejea, baada ya mapigano ya mwishoni mwa wiki iliyopita. Hakuna mapigano Alhamisi hii Julai 14 kwa siku ya tatu mfululizo.

Jeshi la Uganda katika msafara wa kijeshi likielekea Juba, Julai 14, 2016.
Jeshi la Uganda katika msafara wa kijeshi likielekea Juba, Julai 14, 2016. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Lakini nchi nyingi za kigeni zimeendelea kuwarejesha nyumbani raia wao. Na Alhamisi hii asubuhi, msafara wa majeshi ya Uganda umeingia katika ardhi ya Sudan Kusini, ukiwa na sababu rasmi, kuwarejesha nyumbani raia wa Uganda.

Askari zaidi ya mia moja na malori hamsini kutoka Uganda wameingiakatika ardhi ya Sudan Kusini Alhamisi hii Julai 14. Hatua hiyo ilitangazwa siku moja kabla, na msafara ulichelewa kutokana na uamuzi wa Serikali ya Sudan Kusini kufunga mipaka yake.

"Vikosi vyetu vya vya jeshi viko njiani vikieleea katika mji wa Nisitu, kilomita 30 ana mji wa Juba. Hatuna nia ya kwenda mbali zaidi ya mji wa Nisitu, wala nia ya kwenda hadi katika mji wa Juba. Tayari kuna raia 2,000 wawa Uganda ambo wanasubiri kurejeshwa nyumbani. Tunaamini kwamba operesheni hii itadumu siku 10, hadi 20, "amesema msemaji wa serikali ya Uganda.

Kuhusu muda wa operesheni, kumekua na hisia tofauti. Afisa wa Idara ya Ujasusi ya Uganda amelielezea shirika la habari la AFP kwamba vikosi vya jeshi la Uganda vnaweza kukaa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa mjini Juba, na kuongeza, "tumefanya hivyo katika siku za nyuma, kwa nini tusifanyi hivyo kwa sasa? "

Marekani kwa upande wake, tayari imetangaza kwamba imewatuma askari47 katika mji wa Juba, "kulinda raia na mali ya Marekani." Serikali ya Marekani imeongeza: "kwa sasa mjini Djibouti, askari wa ziada wako tayari kutumwa nchini Sudan Kusini kama itahitajika. "