Ufaransa yapendekeza askari 228 kupelekwa Burundi
Ufaransa jana Ijumaa imewasilisha rasimu ya azimio kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa wito wa Kupeleka polisi wapatao 228 wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi kufuatilia haki za binadamu na kusaidia kukomesha mapigano katika nchi za Afrika.
Imechapishwa:
Rasimu hiyo iliyopatikana na AFP inasema kikosi hicho cha askari hao kitapelekwa Bujumbura na nchi nzima ya Burundi Katika kipindi cha awali cha mwaka mmoja, lakini idadi hiyo na mamlaka vitabadilika ikiwa vurugu zitaongezeka.
Bado haijafahamika ikiwa serikali ya Burundi itaridhia pendekezo hilo, na kutoa idhini ya kikosi hicho kupelekwa, hatua ambayo itahitajika na Umoja wa Mataifa ili kutekeleza pendekezo hilo.
Bujumbura imesema hawatakubali zaidi ya maafisa 50 wa polisi wa Umoja wa Mataifa lakini mazungumzo yanaendelea kuhusu mapendekezo ya kupelekwa kikosi kikubwa.
Urusi na Misri wamesema watasaidia kikosi cha polisi cha Umoja wa Mataifa ikiwa tu serikali ya Bujumbura itakubali kupelekwa kwake.