RWANDA-AU

AU yatoa pasi mpya za kusafiria, wawakilishi wa Burundi wakacha mkutano

Rais wa Rwanda, Pual Kagame (kushoto) na rais Idris Deby (Kulia) wakikabidhiwa pasi mpya za kusafiria ambazo zitakuwa ni moja kwa bara la Afrika, 17 Julai, 2016
Rais wa Rwanda, Pual Kagame (kushoto) na rais Idris Deby (Kulia) wakikabidhiwa pasi mpya za kusafiria ambazo zitakuwa ni moja kwa bara la Afrika, 17 Julai, 2016 DR

Bara la Afrika limezindua rasmi Pasi ya kusafiria, inayofahamika kama Passiport ya Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza toka ilipokubaliwa na wakuu wa nchi kwenye mkutano wa 50 wa umoja wa Afrika, ambapo sasa, kutakuwa na pasi moja ya kusafiria kwa wananchi wa bara la Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika, Dr Nkosazana Dlamini Zuma, ametangaza kuwa, Marais wote waliohudhuria kongamano hilo watapewa pasi hiyo kabla ya kukamilika kwa kongamano.

Nkosazana ameongeza kuwa baada ya viongozi wote kupewa pasi hizo za kusafiria, jukumu lina baki kwao kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2018, wananchi wao, wawe wameanza kutumia pasi hizo.

Nae mwenyeji wa mkutano Rais Paul Kagame amesema "umoja barani afrika ndio chanzo cha mafanikio yote ya bara hilo, bara hili likiwa na umoja kila kitu kitawezekana".

Mbali na kuzinduliwa kwa pasi hiyo, mwenyekiti wa umoja wa Afrika Raisi Idris Deby, amekemea vikali hali za ukiukaji wa haki za binaadamu kwenye nchi za Afrika kama vile Burundi na Sudan Kusini, na kuwaomba viongozi wa ichi hizo kuheshimu mikataba ya Amani.

Taarifa zillizothibitishwa na kamati ya umoja wa Afrika, ni kwamba wawakilishi wote kwenye mkutano huo kutoka Burundi wameamua kurudi nyumbani kwa kile walichodai ni kukerwa na matamshi ya kiongozi huyo.