BURUNDI

Mfumuko wa bei, kushuka kwa thamani ya faranga ni kilio kwa Warundi

Mfano wa noti ya faranga 20 ya Burundi.
Mfano wa noti ya faranga 20 ya Burundi. DR

Mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya sarafu ya Burundi, vimesababisha ugumu wa maisha kwa raia wa taifa hilo, athari ambayo imeanza kushuhudiwa hata katika nchi Jirani.

Matangazo ya kibiashara

Wakiongea na RFI Kiswahili, baadhi ya raia wa Burundi wamesema kuwa kwa sasa hali
ya maisha ni ngumu kufuatia faranga yao kumepoteza thamani inapobadilishwa kwa dola ya Marekani na hata shilingi ya Tanzania.

Athari za faranga ya Burundi kupoteza thamani na kusababisha mfumuko wa bei si kwa warundi tu bali hata wenyeji wa nchi jirani.

Baadhi ya raia wa Burundi wamesema kuwa, sababu nyingine zinazosababisha ugumu wa maisha ni pamoja na hali mbaya ya kisiasa nchini mwao.

Aidha maafisa wa Tanzania maeneo ya mpakani ambao hawakupenda kurekodiwa, wamesema kuwa kwasasa bidhaa zinazokwenda Burundi zimepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.

Raia wa Burundi hususani maeneo ya mpakani hutegemea zaidi vyakula na
bidhaa nyingine kwa maisha ya kila siku kutoka upande wa Tanzania, ambapo kwa sasa Tanzania imepiga marufuku mazao ya vyakula kutovushwa mipakani.