SUDAN KUSINI

Maelfu ya raia wa Sudan Kusini wakimbilia Uganda

Wakimbizi wa Sudan Kusini waliyoyakimbia makwao
Wakimbizi wa Sudan Kusini waliyoyakimbia makwao Beatrice Mategwa/United Nations Mission in South Sudan (UNMISS)

Umoja wa Mataifa unasema raia wa Sudan Kusini 37,000 wamekimbia makwao kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita kutokana na mapigano kati ya wanajeshi wanaomtii rais Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar jijini Juba.

Matangazo ya kibiashara

Tume ya Umoja wa Mataifa ya kutetea wakimbizi UNHCR imesema idadi kubwa ya raia hao wa Sudan Kusini wamekimbilia nchi jirani ya Uganda.

Aidha, imebainika kuwa asilimia 90 ya raia hao waliyakimbia makwao ni wanawake na watoto.

Watu hao wamekimbia kutoka jijini Juba, na wale wanaosihi katika jimbo la Eastern Equaitorial.

Kwa sasa raia hao wamefikia katika eneo la Elegu Kaskazini mwa Uganda, ambapo zaidi ya wakimbizi 11,0000 walikuwa wanaishi katika kambi iliyotengewa tu wakimbizi 1000.

UNCHR inaomba wahisani mbalimbali duniani kujitokeza kuwasaidia wakimbizi hao.

Mbali na wakimbizi hao, wengine zaidi ya 831,582 wamekimbilia nchini Ethiopia, Sudan na Uganda.