SUDAN KUSINI

Rais Kirr amtagaza Jenerali Gai kuwa Makamu wa kwanza wa rais

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Stringer

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametangaza kumteua Jenereli Taban Deng Gai kuwa Makamu wa kwanza wa rais kuchukua nafasi ya Riek Machar ambaye aliondoka jijini Juba mapema mwezi huu baada ya kuzuka kwa mapigano mapya.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inadhirisha wazi mgawanyiko kati ya wanasiasa wa upinzani wa SPLM-IO wanaoongozwa na Machar ambaye hajulikani aliko.

Uteuzi wa Gai unakuja wiki moja tu baada ya Machar kumfuta kazi kama Waziri wa madini baada ya kuonekana kushirikiana kwa karibu na upande wa Kiir.

Wanajeshi zaidi ya 100 wa upinzani wamejitokeza kumuunga mkono Deng katika uteuzi huu.

Jenerali Taban Deng Gai
Jenerali Taban Deng Gai Upper Nile Times

Mshirika wa karibu wa Machar, akizungumza mwishoni mwa juma lililopita alisema Machar na viongozi wengine wa upinzani hawajaridhia hatua hiyo na wanaona ni kama ni usaliti kwa upianzani.

Deng akizungumza mwishoni mwa wiki lililopita naye alisema anashikilia nafasi hiyo kwa muda tu na ikiwa Machar atarejea Juba, atamkabidhi Ofisi yake.

Kabla ya kuteuliwa katika wadhifa huu, Deng aliwahi kuwa Gavana wa jimbo la Unity lenye utajiri wa mafuta lakini pia aliongoza waasi katika mazungumzo ya amani mwaka uliopita jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.