UFARANSA-KENYA-TANZANIA

Jean-Marc Ayrault ziarani Kenya na Tanzania

Waziri wa mambo ya Kigeni wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, Juni 15, 2016 Paris.
Waziri wa mambo ya Kigeni wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, Juni 15, 2016 Paris. REUTERS/Jacky Naegelen

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, anafanya ziara ya kikazi Jumatatu hii Agosti 1 nchini Kenya na Jumanne Agosti 2 nchini Tanzania ambapo atakutana na viongozi wa nchi hizi mbili za Afrika Mashariki.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya viongozi hao yatagubikwa na mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi hizi mbili na Ufaransa ambayo bado yako katika ngazi ya kawaida.

Biashara kati ya Ufaransa na Kenya, Ufaransa na Tanzania, inanufaisha upande mmoja, ambao ni Ufaransa. Mwaka 2015, Kenya iliingiza Euro milioni 186 za bidhaa kutoka Ufaransa. Kenya ni mteja nambari moja wa Ufaransa katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa bidhaa za kemikali, uturi na vipodozi ikiwa juu karibu 60% ya mauzo ya Ufaransa kwa Ukanda.

Tanzania iliingiza milioni 160 za bidhaa za Ufaransa, ambapo sehemu kubwa ikihusu dawa. Hata hivyo, katika nchi ambazo zinaonekana katika miaka ya hivi karibuni kuwa na kiwango cha ukuaji muhimu zaidi, 6.5% nchini Tanzania, Kenya 5%, uwepo wa makampuni ya Ufaransa bado ni mdogo sana. Makampuni sitini Kya Ufaransa yanafanya kazi nchini Kenya, na arobaini nchini Tanzania.

Pamoja na ukuaji mkubwa wa mauzo bidhaa kutoka China na India kwenda Afrika ya Mashariki, kiwango cha soko la makampuni ya Ufaransa ni % 1.4 tu nchini Kenya na 0.4% nchini Tanzania.