BURUNDI-CAR-UN

Polisi wa Burundi waondoka CAR

Polisi wa Burundi wakitumia gesi ya kutoa machozi kwa kuwatawanya waandamanaji, Jumapili Aprili 26 Bujumbura.
Polisi wa Burundi wakitumia gesi ya kutoa machozi kwa kuwatawanya waandamanaji, Jumapili Aprili 26 Bujumbura. REUTERS/Thomas Mukoya

Serikali ya Burundi imetangaza Jumatatu hii kwamba inawaondoa polisi wake wote waliotumwa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati. Karibu askari polisi 126 wamewasili Jumatatu hii mchana mjini Bujumbura kwa ndege ya Ethiopian Airlines.

Matangazo ya kibiashara

Kundi jingine la askari polisi 280 ambao wamehudumu kwa mwaka mmoja na miezi kumi sasa mjini Bangui walikua wanatarajiwa kuwasili mjini Bujumbura Jumatatu hii jioni.

Askari polisi 10 pekee ndio watabaki nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa ulinzi wa vifaa vya kivita.

Msemaji wa polisi ya Burundi Pierre Nkurukiye amesema kuwa wamekamilisha kazi yao kwa kuwalindia usalama raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mwezi Juni, Umoja wa Mataifa ulitangaza kwamba hautoongezea muda kwa askari polisi wa Burundi wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji mbalimbali na vitendo vingine vinavyohusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi kabla ya kutumwa katika nchi mbalimbali kusimamia amani.

Baada ta makabiliano Jumamosi Machi 8, hatimaye wafuasi wengi wa chama cha upinzani cha MSD.
Baada ta makabiliano Jumamosi Machi 8, hatimaye wafuasi wengi wa chama cha upinzani cha MSD. RFI / Esdras Ndikumana