Fahamu changamoto za unyonyeshaji maziwa ya mama

Sauti 09:54
Unyonyeshaji wa maziwa ya mama unahamasishwa duniani kote ili kusaidia ukuaji mzuri wa watoto
Unyonyeshaji wa maziwa ya mama unahamasishwa duniani kote ili kusaidia ukuaji mzuri wa watoto hivisasa.co.tz

Unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee ni muhimu katika ukuaji na maendeleo ya mtoto na huchangia kupunguza vifo ya watoto chini ya miaka mitano kwa asilimia 20. Ripoti mbalimbali zinaonyesha ulishaji maziwa ya mama pekee kwa watoto chini ya miezi sita imekuwa tatizo kubwa kwa wanawake walioajiriwa au kujiajiri na uanzishaji wa lishe mbadala ndio chanzo kikubwa cha magonjwa ya utotoni na ukubwani.