Mchango wa Ufaransa kuhimiza amani nchini Burundi, Somalia na Sudan Kusini

Sauti 10:15
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, akizungumza kwenye mahojiano maalumu na rfikiswahili, Agosti 2, 2016.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, akizungumza kwenye mahojiano maalumu na rfikiswahili, Agosti 2, 2016. Emmanuel Makundi/RFI

Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault amekuwa ziarani nchini Kenya na Tanzania. Ziara hii ililenga kujadiliana kuhusu maswala ya biashara na kuimarisha uhusiano kidiplomasia kati ya Ufaransa na nchi hizi mbili za Afrika Mashariki. Ufaransa imesema itaongeza mara mbili msaada wake wa kifedha kwa mataifa hayo ili kufanikisha miradi ya umeme, uboreshaji wa miji na usafirishaji. Ni ziara inayokuja wakati huu mataifa jirani kama Sudan Kusini, Somalia na Burundi yakiendelea kukabiliana na tatizo la usalama na mizozo ya kisiasa. Ufaransa ina jukumu gani kusaidia hizo kupata amani?