BURUNDI-VYOMBO VYA HABARI

Shahidi katika kesi ya Jean Bigirimana atoweka

Askari wa Burundi wakipiga doria katika mitaa ya Bujumbura, baada ya shambulio la guruneti, Februari 3, 2016.
Askari wa Burundi wakipiga doria katika mitaa ya Bujumbura, baada ya shambulio la guruneti, Februari 3, 2016. © REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimama

Kwa mujibu wa muungano wa wanahabari nchini Burundi (SOS Média Burundi), vikimnukuu Pacifique Nininahazwe, kiongozi wa muungano wa mashirika ya kiraia FOCODE, Abel Ahishakiye, mkazi wa wilaya ya Bukeye, mkoani Muramvya, na mtoa habari kwa Idara ya Upelelezi nchini Burundi (SNR) ametoweka tangu wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Abel Ahishakiye anachukuliwa na mashirika yanayotetea haki za binadamu nchini Burundi kama muhusika mkuu katika utekaji nyara wa mwandishi wa habari wa gazeti la Iwacu, ambaye alitoweka wiki tatu zilizopita.

Kwa mujibu wa utafiti uliyopewa jina la "Finding Jean" unaoendeshwa na gazeti la Iwacu, Bw Ahishakiye bila shaka ni muhusika muhimu wa kiutoweka kwa mwenzetu Jean Bigirimana, mwandishi wa habari wa gazeti la Iwacu. Abel Ahishakiye anatajwa kuwa mtu aliyempigia simu mwanahabari huyo ili wakutane sehemu moja wilayani Bugarama kabla ya mwanahabari huyo kutekwa nyara.

"Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Abel Ahishakiye mkazi wa wilaya ya Bukeye alimuitwa kwa simu Jean Bigirimana muda mfupi kabla ya kutekwa nyara. Ni mtoa habari kwa Idara ya Upelelezi (SNR)", gazeti la Iwacu liliandika, na kubaini kuwa mtu huyo alihusika katika kumteka nyara mwandishi wa gazeti hilo, Jean Bigirimana.

Gazeti la Iwacu linasema kuwa abel Ahishakiye alionekana kuwa na vitisho baada ya kukanusha kuwa hamtambui Jean Bigirimana, na kusema kuwa anaitwa Alexis.

Watetezi wa haki za binadamu mkoani Muramvya hawathibitishi wala kukanusha kutoweka kwa Abel Ahishakiye.

Majirani wa Ahishakiye wanasema kuwa siku kadhaa zimepita hawajamuona akirudi nyumbani.

Antoine Kaburahe, Mkurugenzi wa gazeti la Iwacu, Mei 19, 2005  Bujumbura.
Antoine Kaburahe, Mkurugenzi wa gazeti la Iwacu, Mei 19, 2005 Bujumbura. AFP PHOTO / JENNIFER HUXTA