KENYA-UGANDA

Wakuu wa polisi nchini Kenya na Uganda wazuru Kisiwa cha Migingo

Joseph Boinett( Katikati )akisalimiwa na polisi wa Uganda, akiangaliwa na Kale Kayihura (Kulia)
Joseph Boinett( Katikati )akisalimiwa na polisi wa Uganda, akiangaliwa na Kale Kayihura (Kulia) Kenya Police

Wakuu wa jeshi la Polisi nchini Kenya na Uganda wamezuru kisiwa cha Migingo kinachowaniwa na nchi hizo mbili katika Ziwa Victoria.

Matangazo ya kibiashara

Joseph Boinnet kutoka Kenya na Kale Kayuhura wa Uganda wamekutana na wakaazi wa kisiwa hicho na kuwa na kikao cha pamoja cha usalama.

Baada ya ziara hiyo, wakuu hao wa polisi wamekutana jijini Nairobi kuendelea na mazungumzo zaidi ya kiusalama kati ya nchi hizo mbili za Afrika Mashariki.

Wavuvi kutoka Kenya wamekuwa wakilalamika kunyanyaswa na polisi wa Uganda wanapoendelea na shughuli zao za uvuvi, na samaki wao kuchukuliwa suala ambalo lilisababisha pakubwa kuwepo kwa ziara hii.

Kwa muda mrefu sasa, Uganda imekuwa ikisema ardhi katika Kisiwa hicho ni ya Kenya lakini maji ni yake, huku Kenya ikisema Kisiwa chote ni chake kutokana na utajiri wa samaki.

Idadi ya watu kwenye Kisiwa hichi chenye Kilomita ya mraba 2,000 ni 131 kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2009.