Pata taarifa kuu
DADAAB-KENYA-SOMALIA

UNHCR: Wakizimbizi wa Somalia zaidi ya elfu 24 warejea nyumbani

Sehemu ya wakimbizi wa Somalia walioa kurejea nyumbani kwa hiari.
Sehemu ya wakimbizi wa Somalia walioa kurejea nyumbani kwa hiari. unchr.org
Ujumbe kutoka: Emmanuel Richard Makundi
1 Dakika

Wakimbizi wanaokadiriwa kufikia elfu 24 raia wa Somalia waliokuwa wanaishi kwenye kambi ya Dadaab iliyoko kaskazini mashariki mwa Kenya, wamerejea nyumbani, huku wengi wakiamua kurejea kwa hiari. 

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa makabiadhiano ya mtambo maalumu wa kufua umeme kwenye kambi hiyo, naibu mwakilishi wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR kwa nchi ya Kenyam Wella Kouyou, amesema mwaka 2016 pekee wakimbizi elfu 18 wamerejea kwa hiari nchini mwao.

Mapema mwaka huu, Serikali ya Kenya ilitangaza kuwa itaifunga kambi ya Dadaab, kwa kile ilichodai kuwa imekuwa kitovu cha maficho ya wahalifu wanaotekeleza mashambulizi ya ugaidi nchinik humo.

Nchi ya Kenya imekuwa ikishuhudia mfululizo wa mashambulizi yanayotekelezwa na wapiganaji wa Al-Shabab.

Miongoni mwa shambulio baya zaidi kuwahi kutekelezwa na wapiganaji hao, ni lile la shambulio katika chuo kikuu cha Garissa mwezi April mwaka 2015 ambapo wanafunzi zaidi ya 140.

Kouyou amesema kuwa, UNHCR itaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha wakimbizi wanarejea Somalia kwa hiari na wanapewa ulinzi watakapikuwa huko.

"Tutahakikisha kuna kuwa na programu maalumu kwaajili ya ushauri wa wakimbizi wanaorudi." alisema Kouyou.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu mara kadhaa wameionya Serikali dhidi ya kutumia nguvu kuwarudisha nyumbani raia wa Somalia, wakisema kuwa nchi hiyo bado haina usalama.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.