Wanasiasa nchini Kenya wakubaliana kuhusu muundo wa Tume mpya ya Uchaguzi

Sauti 10:21
Nembo ya Tume huru ya uchaguzi nchini Kenya IEBC
Nembo ya Tume huru ya uchaguzi nchini Kenya IEBC ebru

Wanasiasa wa serikali na upinzani nchini Kenya wamekubaliana kuhusu muundo mpya wa Tume ya Uchaguzi nchini humo kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2017. Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kuwepo kwa Makamishena wapya saba lakini pia kupitiwa upya kwa daftari la wapigia kura. Wakenya wanatoa mtazamo wao kuhusu makubaliano hayo ikiwa wanaamini kuwa yanaweza kusaidia nchi hiyo kuwa na uchaguzi utakaokuwa huru na haki.