SUDANI KUSINI

Ripoti ya siri ya UN yasema Salva Kiir na mkuu wa majeshi waliamuru mapigano ya Julai 8 nchini Sudan Kusini

Raisi wa Sudani kusini Salva Kiir
Raisi wa Sudani kusini Salva Kiir REUTERS/Stringer

Ripoti ya siri ya Umoja wa Mataifa imebaini kwamba mapigano mapya yaliyozuka hivi karibuni katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kuanzia tarehe 8 Julai yaliamuriwa na Rais Salva Kiir na mkuu wa majeshi, Paul Malong Awan. 

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo pia imebaini kuwa jeshi la Rais Kiir lilileta magari yaliyojazwa silaha kutoka nchi jirani ya Uganda mwezi Juni, siku au majuma kadhaa kabla ya mapigano kuanza katika juma la kwanza la mwezi Julai katika ukumbi wa Rais.

Jopo la uchunguzi la Umoja wa Mataifa pia limesema kikundi cha upinzani wakiongozwa na aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Riek Machar, hawakununua silaha kabla ya mapigano hayo.

Ripoti hiyo imetolewa huku kukiwa na hali ya wasiwasi miongoni mwa wanaharakati wa demokrasia nchini Sudan Kusini ambao walikutana na wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Juma hili wanaoripitiwa kutoroka nchi hiyo kwa hofu ya usalama wao.

Edmond Yakani, Mkuruenzi Mkuu wa Mashirika ya Kiraia jijini Juba ametibitisha kuanza kuotoka nchini humo kwa baadhi ya wanaharakati hao baada ya kukutana na wajumbe wa Baraza hilo wiki hii.

Aidha,amesema kuwa tangu kufanyika kwa mkutano huo mwanaharakati mwenzao Emmanuel Wani, ameauawa baada ya kupigwa risasi suala ambalo limezua hofu kati yao.