Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Ripoti yaeleza namna rais Salva Kiir, Riek Machar walivyojitajirisha kutokana na vita

Rais wa Sudan Kusini (Kulia) na aliyekuwa Makamu wake Riek Machar (Kushoto)
Rais wa Sudan Kusini (Kulia) na aliyekuwa Makamu wake Riek Machar (Kushoto) REUTERS/Stringer
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
1 Dakika

Wanasiasa maarufu na viongozi wa kijeshi nchini Sudan Kusini wamejitajirisha kutokana na mzozo wa kisiasa na usalama unaoendelea katika nchi yao.

Matangazo ya kibiashara

Hii imebainika katika ripoti maalum iliyotolewa na Mwigizaji kutoka nchini Marekani George Clooney, inayozungumzia kujitajirisha kupitia vita.

Katika ripoti hiyo, Clooney anamshutumu rais Salva Kiir na kiongozi wa upinzani Riek Machar kuwa viongozi wa juu waliojitajirisha kutokana na mzozo huo.

Ripoti hii inaeleza kuwa familia za rais Kiir na Machar, zimejipatia kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mzozo huu.

Rais Kiir na Machar hawajajitokeza kujibu tuhma hizi dhidi yao, katika ripoti hii inayowatuhumu pia kuhusika moja kwa moja na mauaji na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za kibinadamu.

Aidha, ripoti hii imeeleza kuwa viongozi hao wa kisiasa wanamiliki mali na kuishi maisha ya kifahari wanapokuwa nchini Kenya, Uganda na Australia.

Ripoti hii imekuja baada ya kuzuka kwa vita nchini humo mwaka 2013, wakati vikosi vinavyomtii rais Kiir na Machar vilipoanza kukabiliana jijini Juba.

Maelfu ya watu wamepoteza maisha na Mamilioni kuyakimbia makwao kutokana na mzozo huu .

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.