Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA

Human Rights Watch yasema Kenya inawalazimisha wakimbizi kurudi Somalia

Kambi ya wakimbizi ya Daadab kaskazini mwa nchi ya Kenya, inayohifadhi wakimbizi wa Somalia
Kambi ya wakimbizi ya Daadab kaskazini mwa nchi ya Kenya, inayohifadhi wakimbizi wa Somalia UNHCR - kenya
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
1 Dakika

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, linasema kuwarudisha nyumbani wakimbizi raia wa Somalia wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Daadad Kaskazini Mashariki mwa Kenya ni kinyume cha sheria na utaratibu wa Kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii imekuja wakati huu serikali ya Kenya ikiendelea na zoezi la kuwarudisha nyumbani maelfu ya wakimbizi ambao wamekuwa wakiishi katika kambi hiyo.

Human Rights Watch inasema imewahoji zaidi ya wakimbizi 100 ambao wamekiri kuwa wanarudi nyumbani kwa sababu wanahofia kurudishwa kwa nguvu na serikali ya Kenya.

Aidha, Shirika hilo linadokeza kuwa wakimbizi hao wanaorudi Somalia wanahofia kupoteza maisha, kuteswa na kukabiliwa na baa la njaa wanapofika nchini mwao.

Serikali ya Kenya tayari imetangaza kuwa itafunga kambi hiyo kubwa duniani yenye wakimbizi 266,000 kutoka Somalia itafungwa ifikapo mwezi Novemba mwaka huu kwa sababu za kiusalama.

Wakimbizi hao sasa wanahofia kuwa huenda wakakosa Dola 400 kama malipo ya kurudi nyumbani kwa madai kuwa serikali ya Kenya haiwapi taarifa kuhusu kusalia kwao katika kambi hiyo lakini pia hali ya mambo nchini Somalia.

Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kimataifa yamekuwa yakitoa wito kwa serikali ya Kenya kutowalazimisha wakimbizi hao kurudi nyumbani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.