ZANZIBAR-MALAYSIA

Kipande cha ndege kilichopatikana Visiwani Zanzibar ni cha ndege ya Malaysia MH370 iliyotoweka

Malaysia imethibitisha kuwa kipande cha ndege kilichopatikana Pwani ya kisiwa cha Pemba, Visiwani Zanzibar  nchini Tanzania mwezi Juni mwaka huu, ni ya ndege ya abiria iliyotoweka ya MH370 mwaka 2014.

Kipande cha ndege ya Malaysia MH370 iliyotoweka  mwaka 2014.
Kipande cha ndege ya Malaysia MH370 iliyotoweka mwaka 2014. REUTERS/Zinfos974/Prisca Bigot
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Uchukuzi nchini humo imesema baada ya uchunguzi wa kina, imebaini kuwa ni kweli kipande hicho ni cha ndege hiyo ambayo imekuwa ikitafutwa kwa muda mrefu bila mafanikio.

Hata hivyo, Wizara hiyo imesema kuwa watalaam wanaendelea na uchunguzi wa kina ili kujaribu kupata ukweli kuhusu ilikopotelea ndege hiyo.

Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 239, ilitoweka tarehe 8 mwezi Machi mwaka 2014, ikitokea jijini Kuala Lumpur nchini Malaysi a kwenda jijini Beijing nchini China.

Wataalam wanaamini kuwa ndege hiyo iliyoanguka katika Bahari Hindi.