KENYA-ICC

ICC yatoa malalamiko yake kwa nchi wanachama

Mwendesha mashitaka Fatou Bensouda alisitisha mashtaka yake dhidi ya Uhuru Kenyatta.
Mwendesha mashitaka Fatou Bensouda alisitisha mashtaka yake dhidi ya Uhuru Kenyatta. Getty Images

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imeamua Jumatatu hii kufikisha malalamiko yake kwa baraza la nchi wanachama (ASP) wa ICC, ya kukosekana kwa ushirikiano wa Serikali ya Kenya.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Nairobi ilikataa kukabidhi taarifa za benki na rekodi ya simu, ambavyo kwa mujibu wa ICC, vingeliweza kuthibitisha hatia ya rais wa Kenya.

Majaji wanasema kuwa Kenya haikutimiza majukumu yake ya ushirikiano na wanaamini kwamba Baraza hilo lina nafasi nzuri ya kushughulikia suala hilo la kukosekana kwa ushirikiano.

Mwaka 2013, upande wa mashtaka uliomba ICCkuamua kwamba Kenya ilikiuka wajibu wake wa ushirikiano.

"Serikali ya Kenya ilikataa kukabidhi taarifa za benki na rekodi ya simu, ambavyo vingeliweza kuthibitisha hatia ya rais wa Kenya, " ICC imebaini katika taarifa yake.

Mwendesha mashitaka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Fatou Bensouda, alisitisha mashtaka yake dhidi ya Uhuru Kenyatta mwaka 2014 kwa kukosa ushahidi wa madai ya makosa yaliyotokea katika vurugu za baada ya uchaguzi za mwishoni wa mwaka 2007-2008.