BURUNDI-UN

Burundi yakashifu ripoti ya wachunguzi wa UN, yasema imejaa upendeleo

Maandamano ya hivi karibuni ya raia wa Burundi nchi ya Ubalozi wa Ufaransa mjini Bujumbura, walikuwa wakikashifu Jumuiya ya Kimataifa.
Maandamano ya hivi karibuni ya raia wa Burundi nchi ya Ubalozi wa Ufaransa mjini Bujumbura, walikuwa wakikashifu Jumuiya ya Kimataifa. STR / AFP

Serikali ya Burundi inautuhumu umoja wa Mataifa kwa kuwa na ubaguzi na upendeleo, ikidai kuwa wachunguzi wake walioenda nchini humo hivi karibunim walisukumwa kisiasa na hitimisho la ripoti yao liliegemea ushahidi wa watu wasiojulikana wala kuthibitishwa.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya umoja wa Mataifa imesema kuwa, Serikali ya Burundi inahusika na matukio ya kupangwa ya ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwemo mauaji na mateso, imesema ripoti hiyo na kuonya kuhusu uwezekano wa kutokea mauaji ya halaiki.

Serikali ya Burundi imesema kuwa, haikutarajia kuona ripoti tofauti ikitolewa na wachunguzi hao wa umoja wa Mataifa, ambao imesisitiza walikuwa nchini humo kwa sababu za kisiasa na hawakuzingatia ushahidi na maelezo yaliyotolewa na Serikali wakati wakihitimisha uchunguzi wao.

Burundi inasema hii si mara ya kwanza kwa umoja wa Mataifa kutengeneza kile ilichoita ni uongo kuhusu nchi hiyo, na kuongeza kuwa wahusika wa mgogoro na mauaji nchini humo wanajulikana, lakini badala yakle tume ya uchunguzi ikaamua kuinyooshea kodole cha moja kwa moja Serikali yao.

Ripoti hiyo ya jopo la wachunguzi huru watatu, imesema kuwa matukio makubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu yametekelezwa na yanaendelea kutekelezwa nchini humo, vitendo vinavyofanywa na maofisa wa Serikali pamoja na washirika wake.

Wachunguzi hao wameongeza kuwa, kamwe hawawezi kujitenga na ukweli kuwa, baadhi ya matukio hayo ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanaweza kufikia kiwango cha uhalifu dhidi ya binadamu.

Jopo hilo la uchunguzi liliundwa na tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa mwezi January mwaka huu, kuchunguza matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Burundi toka kuanza kwa machafuko nchinik hujmo mwezi April mwaka jana, baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu, katika kura aliyoshinda kwenye uchaguzu wa mwezi Julai.

Tume hiyo baada ya kufanya safari mbili nchinik Burundi na kuwahoji watu zaidi ya 227, wachunguzi hao walianisha picha hali ambayo wamesema watu zaidi ya elfu moja wameuawa toka kuanza kwa machafuko nchini humo.

Tume ya haki za binadamu imethibitisha mauaji ya watu 564 yaliyokuwa ya kupangwa katik ya April 26, 2015 na tarehe 30 ya mwezi Agosti 2015, huku ripoti hii ikihitimisha kwa kudai kuwa mauaji hayo yalikuwa yamekadiriwa vema.