UGANDA-SIASA-UCHUMI

Sherehe za kutunukiwa medali wabunge 1000 zafanyika Uganda

Jengo la Bunge la Uganda
Jengo la Bunge la Uganda CC/Andrew Regan

Bunge nchini Uganda limeandaa sherehe jijini Kampala hivi leo, kutunukiwa medali wabunge wa zamani na wa sasa kwa kile ambacho bunge linasema ni kutambua juhudi zao za kuwafanyia kazi raia wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Spika wa bunge Rebeca Kadaga amesema zaidi ya wabunge 1000 wanatarajiwa kutunukiwa medali hizo, akiwemo mwanasiasa mkongwe wa upinzani Kizza Besigye pamoja na mkewe.

Hata hivyo, idadi kubwa ya raia wa Uganda wanakosoa mpango huu wa bunge kwa kile wanachosema ni matumizi mabaya ya fedha za umma ambazo zingetumiwa kufanya miradi ya maendeleo.

Pamoja na hilo, raia wengi wanasema hawaoni chochote ambacho kimefanywa na wabunge hao.