BURUNDI-USALAMA

Jopo la wataalamu wa UN kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu Burundi

Wakimbizi wa Burundi wakiwa katika kambi ya wakimbizi Nduta Kigoma nchini Tanzania.
Wakimbizi wa Burundi wakiwa katika kambi ya wakimbizi Nduta Kigoma nchini Tanzania. AFP Photo/Oxfam/Mary Mndeme

Umoja wa mataifa umeamua kutuma kikosi cha wataalamu wa kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi baada ya ripoti iliyoonya kuwepo hatari ya kutokea mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la kutetea haki katika umoja wa mataifa UN lilitoa onyo juu ya ghasia za nchini Burundi tangu April 2015 na kupiga kura ya kutuma haraka jopo la wataalamu ambao huundwa tu panapokuwa na hali ya ulazima.

Kwa sasa kuna tume mbili tu za uchunguzi ambazo ziliundwa na UN moja kushughulikia mzozo wa Syria na mwingine Sudan kusini ambayo iliingia vitani mwaka 2013.

Maazimio hayo ya ijumaa yanatoa wito wa kufanyika uchunguzi wa mwaka mmoja juu ya ukiukwaji uliofanyika tangu taifa hilo kuingia katika vurugu mwaka 2015 baada ya uamuzi tata wa raisi Nkurunziza kuwania muhula wa tatu wa uongozi.

Maazimio hayo yaliungwa mkono na umoja wa ulaya na kuidhinishwa kwa kura 19 huku kura 7 zikipinga.