UGANDA-SIASA

Upinzani nchini Uganda wakataliwa kuadhimisha miaka 54 ya uhuru

Uganda ambayo ilikua koloni ya Uingereza, imeadhimisha Jumapili hii, Oktoba 9 miaka 54 ya uhuru. Sherehe rasmi iliyoandaliwa na serikali ilifanyika katika wilaya ya luuka, mashariki mwa nchi. Wakati huo huo, upinzani ulitaka kuandaa sherehe zao wenyewe katika mji mkuu Kampala lakini walijikuta wakikabiliwa na polisi.

Kizza Besigye, mpinzani mkuu wa Museveni. (Picha iliyopigwa Julai 13, 2016).
Kizza Besigye, mpinzani mkuu wa Museveni. (Picha iliyopigwa Julai 13, 2016). ©Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Polisi ilionya upinzani kutothubutu kufanya maadhimisho bila kibali cha serikali , siku chache zilizopita.

"Kufanya mikutano sambamba na maadhimisho ya kitaifa inaonekana kuwa ni vurugu ambazo zinaweza kuhatarisha usalama na maadhimisho rasmi ya leo," polisi imeonya. Wakati huo huo, polisi imesema kuwa iliwaonya raia wanaotaka kujiunga na upinzani katika mkutano huo.

Hata hivyo, chama cha upinzani cha FDC cha Kizza Besigye, kilikuwa kimepanga kukutana ili kuadhimisha miaka 54 ya uhuru katika eneo maarufu la Katwe lakini Jumapili asubuhi, kiongozi wa chama hicho "alichukuliwa na polisi wakati alipokua akijaribu kuondoka nyumbani, " mwanasheria wa chama cha FDC amesema. Kwa siku kadhaa, vikosi vya usalama vilikua vimepiga kambi nje ya makazi ya kiongozi mkuu wa upinzani, wakinyima haki ya kutembea. Polisi wakati huo huo ilikua haipatikani.

Besigye alichukua nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais wa mwezi Februari akipata 35% ya kura. Tangu wakati huo serikali inakabiliana naye kwa kampeni zake za dharau. Kampeni hizo zilisababisha kuwekwa jela kwa miezi miwili.