RWANDA-UFARANSA-USHIRIKIANO

Paul Kagame atishia kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Ufaransa

Mbele ya Bunge Jumatatu Oktoba 10, katika hotuba ya ufunguzi wa mwaka wa mahakama, Rais wa Rwanda Paul Kagame aliitishia Ufaransa kwa kuvunjika upya kwa mahusiano ya kidiplomasia.

Rais wa Rwanda Paul Kagame atishia kwa mara nyingine tena kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Ufaransa.
Rais wa Rwanda Paul Kagame atishia kwa mara nyingine tena kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Ufaransa. REUTERS/Ruben Sprich
Matangazo ya kibiashara

Kauli yake inatokana na ufunguzi, wiki iliyopita, wa uchunguzi kuhusu mauaji ya rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana tarehe 6 Aprili 1994. Ufunguzi huo ulifanywa na majaji wa Ufaransa.

Mauaji hayo yanachukuliwa kama chanzo cha mlipuko wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Washirika saba wa karibu wa Paul Kagame wanahusishwa katika mauaji hayo. Wachunguzi wa Uifaransa wanataka kumsikia Kayumba Nyamwasa, askari wa zamani wa kijeshi wa Rwanda, aliyefarikiana na Rais Paul Kagame na ambaye anamshutumu rais huyo kuwa mwanzilishi wa shambulio dhidi ya ndege ya rais Juvenal Habyarimana.

Tangu mwaka 2012, majaji wa Ufaransa walikua bado wakishikilia tathmini ya shambulizi dhidi ya ndege ya rais Habyarimana kuwa liliendeshwa na Wahutu wenye msimamo mkali. Uchunguzi ulifungwa na walikua wanatarajiwa kuwasikiliza washirika wa karibu wa Rais Paul Kagame, lakini uamuzi wa kumsikiliza afisa wa zamani wa ngazi ya juu katika jeshi la Rwanda Kayumba Nyamwasa unaweka matatani mahusiano ya kidiplomasia kati ya Rwanda na Ufaransa.

Rais wa Rwanda awali alisema hakuwa na tatizo na hilo. Kisha akainua sauti yake akimaanisha njama za Paris katika mauaji ya kimbari.

"Napaswa kuwakumbusha baadhi ya watu yaliyotokea nchini Rwanda, kwamba mfumo wa mahakama ya Rwanda hauko chini ya maslahi ya Ufaransa. Ufaransa ndio inapaswa kuwekwa kizimbani na kuhukumiwa ... na wala si mtu yeyote nchini Rwanda, " amesema rais wa Rwanda.

Paul Kagame hakuishia hapo. Aliwaambia wanadiplomasia na kuwakumbusha, kwamba kuna hatari mahusiano ya kidiplomasia kati ya Ufaransa na Rwanda kuvunjika.

Ufaransa na Rwanda zilivunja mahusiano yao ya kidiplomasia kati ya mwaka 2006 na 2009. Ubalozi wa Ufaransa mjini Kigali ulifungwa, kufuatia vibali vya kukamatwa washirika wa karibu wa Rais Paul Kagame.