BURUNDI-ICC

Makundi ya haki yakashifu kura ya Burundi kujiondoa ICC

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ????

Mashirika ya haki jana Ijumaa yameshutumu kura iliyopigwa na wabunge wa Burundi kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa, ya uhalifu wa kivita ICC yakionya kwamba serikali hiyo inajaribu kuficha ukiukaji wa haki mbele ya macho ya dunia.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa shirika la FIDH linalowakilisha makundi ya haki za binadamu duniani kote Dimitris Christopoulos, amesema kuwa Kama Burundi itajiondoa katika mahakama hiyo itakuwa ishara ya wazi kwa serikali hiyo kuamua kujitenga.

Aidha ameongeza kuwa Jaribio hili la kuinyima jumuiya ya kimataifa kuona na kusikia yanayoendelea nchini Burundi ili kuendelea kufanya uhalifu mkubwa wa haki bila dunia kujua, linahitaji mwitikio imara na wa haraka kutoka kwa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

Siku ya Jumatano wabunge wa Burundi walipiga kura kwa kishindo kujiondoa katika mahakama ya ICC, Hatua inayolifanya taifa hilo kuwa la kwanza kukaribia kujiondoa.
 

Kwa sasa hatua inayongojewa ni kwa rais Pierre Nkurunzinza kuweka saini katika muswada wa kujiondoa kwa nchi hiyo katika mahakama ya ICC ili kuidhinisha rasmi mchakato huo.