EU-BURUNDI-USIRIKIANO

EU kuitenga Burundi kwa fedha za AMISOM

Umoja wa Ulaya umekua ukiitishia serikali ya Burundi kuitenga kwa fedha za kikosi chake kilichotumwa nchini Somalia kujiunga na kikosi cha Umoja wa Afrika kusimamia amani nchini humo (AMISOM). Kwa sasa Umoja wa Ulaya umeanza kuchukua hatua.

Askari wa Burundi wa kikosi cha AMISOM wakipiga doria nchini Somalia (mwezi Oktoba 2013).
Askari wa Burundi wa kikosi cha AMISOM wakipiga doria nchini Somalia (mwezi Oktoba 2013). ABDI DAKAN / AU-UN IST PHOTO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya, mfadhili mkuu wa Burundi unaochangia 20% ya bajeti ya taifa hilo, umeamua kuchukua vikwazo dhidi ya serikali ya Burundi, inayotuhumiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kukataa mpaka sasa kuketi kwenye meza ya mazungumzo na upinzani wake. Lakini mbele ya serikali ambayo imeendelea kutengwa katika ngazi ya kimataifa, na kutuhumiwa uhalifu mbaya dhidi ya binadamu, Umoja wa Ulaya unataka kuzuia moja ya sehemu kuu zinazoipatishia serikali ya Burundi sarafu za kigeni.

Umoja wa Ulaya umechukua uamuzi wa kutopitisha tena mishahara ya askari wa nchi hiyo wanaosimamia amani nchini Somalia kwenye akaunti ya serikali. Hata hivyo uchumi wa Burundi umeendelea kudorora, hata baadhi ya shughili zinazoingiza mapato kwa serikali zimekwama kutokana na hali mbaya ya kiuchumi

Ni wki tatu sasa tangu Umoja wa Ulaya kutuma fedha kwenye akaunti ya Umoja wa Afrika ili kulipa mishahara askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).

Lakini serikali ya Brussels imelipa tu malimbikizo ya kipindi kinachoishia hadi Machi 16, 2016, tarehe ambayo Umoja wa Ulaya uliiwekea vikwazo serikali ya Burundi, kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Mkataba wa Cotonou.

Tangu wakati huo, Umoja wa Ulaya ulisimamisha misaada yake ya moja kwa moja kwa serikal ya Burundi. Lakini kila mwezi, Euro milioni 5 za mishahara ya askari 5,500 wa Burundi wa kikosi cha AMISOM zimekua zikipitishwa kwenye hazina ya serikali ya Burundi. Burundi imekua ikinufaika kupitia fedha hizo.