RWANDA-SIASA

Mfalme wa mwisho wa Rwanda afariki

Picha isiyo na tarehe ya Kigeli wa 5, mfalme wa Rwanda kuanzia mwaka 1959 hadi 1961
Picha isiyo na tarehe ya Kigeli wa 5, mfalme wa Rwanda kuanzia mwaka 1959 hadi 1961 Getty images/Universal History Archive/UIG

Mfalme wa mwisho wa Rwanda, Kigeli wa 5, aliyetimuliwa madarakani tangu miaka hamisini iliyopita, aliishi uhamishoni nchini Marekani tangu mwaka 1992. Mfalme huyo alifariki dunia Jumapili, Oktoba 16, taarifa ambayo imethibitishwa na mmoja wa ndugu zake. Alikuwa na umri wa miaka 80. Mmoja wa ndugu zake atateuliwa kwa kutoa tangazo rasmi kuhusu kifo cha mfalme Kigeli wa 5, aliyefariki mbali na nchi yake.

Matangazo ya kibiashara

Jean-Baptiste Ndahindurwa ni jina lake la ubatizo, alikua na umri wa miaka 23 wakati alikabidhiwa kiti cha enzi mwaka 1959. Wakati huo, Rwanda ilikua chini ya usimamizi wa Ubelgiji, na Mwami, mfalme wa Rwanda, hakua na hadhi yoyote kama watangulizi wake.

Mwaka 1961, Ubelgiji ilianzisha mchakato wa uhuru wa ndani na kura ya maoni ilipigwa. 80% ya Wanyarwanda walipiga kura ya kufuta utawala wa kifalme. Kigeli V, ambaye tangu wakati huo aliishi uhamishoni, hakuhudhuria shereshe za uhuru wa Rwanda, uliotangazwa mwezi Julai 1962.

Mfalme Kigeli wa 5 alihamia nchini Marekani tangu mwaka 1992, baada ya kuishi miaka kadhaa nchini Tanzania, Uganda na Kenya. mwandishi wa habari wa Marekani ambaye ni wa mwisho kukutana naye akiwa ukimbizini anasema mfalme huyo alikua akiishi kwa shida katika kitongoji kimoja mjini Washington kwa misaada ya kijamii ya Marekani na michango kutoka wa raia wa Rwanda waishio ugenini.

Akiwa uhamishoni kwa zaidi ya miaka hamsini, na licha ya wito uliyotolewa na chama cha Green Party nchini Rwanda, Kigeli wa 5 hakupata nafasi ya kuiona tena nchi yake, ambapo alitawala muda mfupi.