SUDAN KUSINI-MACHAR

Machar aahidi kurejea Sudan Kusini

Aliyekuwa makamu wa rais nchini Sudan Kusini Riek Machar Aprili 29, 2014.
Aliyekuwa makamu wa rais nchini Sudan Kusini Riek Machar Aprili 29, 2014. AFP Photo:UNMISS/Isaac Alebe Avoro

Aliyekuwa makamu wa rais nchini Sudan Kusini Riek Machar, aliyeitoroka nchi hiyo na kukimbilia uhamishoni baada ya vita kuzuka katika mji wa Juba mwezi Agosti mwaka huu, ameahidi kurejea nchini mwake hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Bw Machar ametoa kauli hiyo wakati ambapo mapigano makali yameendelea kurindima katika waMalakal kati ya wanajeshi wake na wanajeshi wa serikali.

Kwa mujibu wqa vyombo vya habari vya Afrika Kusini ambapo anapata matibabu, Bw Machar amesema bado anapendwa na idadi kubwa ya wananchi wa Sudan Kusini, na bado kundi la waasi wake wana matumaini ya kutekelezwa moja kwa moja mkataba wa amani ya kudumu na serikali ya Juba.

Itafahamika kwamba baada ya vita vikali kutokea katika mji wa Juba, Riek Machar aliamua kukimbilia uhamishoni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na baadaye alihamia katika mji wa Khartoum, nchini Sudan Kusini.