BURUNDI-EU

Askari wa Burundi kuondoka Somalia

Askari wa Amisom jkatika mji wa Barawe, Somalia, mwezi Oktoba 2014.
Askari wa Amisom jkatika mji wa Barawe, Somalia, mwezi Oktoba 2014. AFP PHOTO/AMISOM/TOBIN JONES

Burundi, ambayo imeendelea kukumbwa na mgogoro kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa, iko chini ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya tangu mwezi Machi kutokana na ukiukwaji mbalimbali wa haki za binadamu na kukataa kuketi kwenye meza ya mazungumzo na upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuamua kuongeza vikwazo vyake kutokana na hali inayoendelea katika nchi hii ya Maziwa Makuu, Umoja wa Ulaya umeamua kuzidisha vikwazo vya kifedha dhidi ya serikali ya Burundi. Ubelgiji, ambayo inafadhili karibu kwa kiwango kikubwa kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM), imeamua kutopitisha kwenye hazina ya serikali mishahara ya askari 5,500 wa Burundi waliojiunga katika kikosi hiki cha Umoja wa Afrika nchini Somalia.

Kwa kusubiri mchakato huo ukamilike, Ubelgiji imeamua kuzuia mishahara ya askari wote kutoka Burundi wanaosimamia amani nchini Somalia. Umoja wa Afrika umekosa la kufanya baada ya uamuzi huo.

Wakati huo huo hati inayotangaza kusimamishwa kwa zoezi la mzunguko wa kushiriki katika kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia kwa askari wa Burundi kutoka bataliani tatu, karibu nusu askari wa kikosi hiki, imekua ikisambazwa tangu Jumanne Oktoba 18 kwenye mitandao ya kijamii. Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Burundi Kanali Gaspari Baratuza ameithibitishia RFI kuwa taarifa hiyo ni sahihi.

Lakini Kanali Gaspard Baratuza, amesema ni jambo la kawaida kabisa kwa sababu imeshatokea mara kadhaa." Kuhusu kwamba uamuzi huu wa ghafla unahusiana na uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kutopitisa kwenye hazina ya serikali mishahara ya askari wa Burundi wakioko Somalia, "hiyo si kazi yetu," amesema msemaji wa jeshi la Burundi.