MOROCCO-TANZANIA

Mfalme wa Morocco ziarani Tanzania

Mfalme wa Morocco Mohammed anafanya ziara ya zaidi ya siku tano nchini Tanzania tangu Jumapili hii Oktoba 23. Aliwasili nchini humo Jumapili hii akiwa na msafara wa ndege tano zilizobeba vitu vyake ikiwa ni pamoja na kitanda na mazulia ya kifalme.

Mfalme wa 6 wa Morocco (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli (kulia). 23 October 2016.
Mfalme wa 6 wa Morocco (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli (kulia). 23 October 2016. Ikulu/Tanzania/Issa Michuzi
Matangazo ya kibiashara

Mfalme Mohammed VI ameambatana na ujumbe wake wa watu 150. Amewasili nchini Tanzania akitokea nchini Rwanda.

Mfalme wa Morocco anatazamiwa kufanya mazungumzo na Rais John Pombe Magufuli Jumatatu hii katik Ikulu jijini Dar Es Salaam.

Mambo yatakayojadiliwa na viongozi hao ni uhusiano baina ya nchi zao na Morocco kutafuta uungwaji mkono ili irejee katika Umoja wa Afrika.

Mfalme Mohammed VI atafanya ziara rasmi ya siku tatau na baadaye ataanza likizo yake na kutumia siku tano zaidi kutembelea vivutio vya utalii.

Hata hivyo serikali za Tanzania na Morocco zitasaini makubaliano mbalimbali ya biashara, ikiwa ni pamoja na mkakati wa nchi hizi kuimarisha uchumi.

Awali Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Augustine Mahiga alisema lengo la ziara hii ni kuanzisha diplomasia ya kiuchumi kwa kuwa Morocco ni moja ya nchi zilizoendelea kiuchumi.