KENYA-AL SHABAB

Kenya; wanamgambo wa Al Shebab hawahusiki katika shambulizi la Mandera

Mji wa Manderawaendelea kukumbwa na mashambulizi ya watu wenye silaha.
Mji wa Manderawaendelea kukumbwa na mashambulizi ya watu wenye silaha. REUTERS

Kwa uchache watu 12 waliuawa katika shambulio la bomu usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne hii katika mji wa Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya. Katika shambulio hilo watu kadhaa walijeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Sehemu moja ya nyumba ya wageni iliporomoka kufuatia mlipuko wa bomu lililotengenezwa kienyeji.

Afisa wa jeshi amesema wanamgambo wa kundi la Al Shabab hawahusiki moja kwa moja katika shambulio hilo, ambalo mapema mchana wanamgambo hao wa Kiislam wa Somalia walikiri kuhusika na shambulio hilo lililotokea katika eneo moja mjini Mandera.

Mohamud Saleh, mratibu wa usalama wa eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya, amesema kuwa uchunguzi wa awali umedhihirisha kuwa shambulio hilo la saa tisa alfajiri lilitekelezwa na "magengi ya wahalifu walio na itikadi kali waliopo katika mji wa Mandera ambao wametumia vilipuzi vinne kuilipia nyumba hiyo ya malazi".

Hili ni shambulio la pili katika Kaunti hiyo katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja.