KENYA-USALAMA

Watu wasiopungua 12 wauawa katika mji wa Mandera

Watu wawili, ambao walinusurika katika mashambulizi ya kundi la Al-Shabab yaliyosababisha vifo vya watu 36 katika eneo la Mandera, Desemba 6 mwaka 2014.
Watu wawili, ambao walinusurika katika mashambulizi ya kundi la Al-Shabab yaliyosababisha vifo vya watu 36 katika eneo la Mandera, Desemba 6 mwaka 2014. REUTERS/Goran Tomasevic

Watu wenye silaha wameshambulia eneo moja la mji wa Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya, watu zaidi ya 12 wanahofiwa kupoteza maisha katika shambulizi hilo. Eneo lililoshambuliwa huishi watu kutoka nje ya mji huo, kwa mujibu wa polisi.

Matangazo ya kibiashara

Haijafahamika waioendesha shambulio hilo lakini polisi ya Kenya inasema milipuko mitano imlisikika kabla ya polisi kukabiliana na kundi hilo.

Hata hivyo polisi imesema imeanzisha msako katika eneo hilo na kushika doria katika mji wa Mandera.
Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, watu wanne wameuawa na wengine kdhaa kujeruhiwa.

Mandera ambao ni mji ulio karibu na mpaka na Somalia umekua ukikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara. Mashambulizi ambayo, kwa mujibu wa vyombo vya usalama vya Kenya yamekua yakitekelezwa na kundi la wanamgambo wa Al-Shabab.

Mwanzoni mwa mwezi huu watu waliojihami kwa silaha walishambulia mtaa mmoja mjini Mandera, nchini Kenya. Wakati huo Mkuu wa jimbo la Mandera Ali Roba aliandika kwenye Twitter kwamba watu 6 waliuawa na mmoja kujeruhiwa.

Usiku wa kuamkia Alhamisi September 22 kundi la wapiganaji wa kiislamu wenye silaha wlishambulia kituo kimoja cha Polisi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo

Msemaji wa jeshi la polisi nchini Kenya, George Kinoti alithibitisha kutokea kwa tukio hili na kuongeza kuwa, wapiganaji zaidi ya 50 waliojihami kwa silaha walivamia kituo cha polisi na polisi waliokuwa doria, ambapo baadae polisi hao walifanikiwa kukabiliana nao.

Itakumbukwa kwamba wanajeshi wa Kenya wamekua wakitumwa nchini Somalia ili kuzima mashambulizi ya mara kwa mara nchini mwake na kuisaidia serikali dhaifu ya Somalia kuimarisha usalama nchini Somalia.