KENYA-USALAMA

Serikali ya Kenya yatangaza amri ya kutotoka nje usiku Mandera

Mji wa Mandera, unaendelea kukumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara.
Mji wa Mandera, unaendelea kukumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara. REUTERS

Katika waraka, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Joseph Nkaisserry amesema amri ya kutotoka nje usiku imetangazwa katika mji wa Mandera na viunga vyake. Watu 12 na waliuawa wengine kadhaa walijeruhiwa katika shambulzi lililotokea wiki hii katika eneo moja la mji wa Mandera.

Matangazo ya kibiashara

Mji wa Mandera, unaopatikana kaskazini mwa Kenya, ulikubwa na shambulizi la bomu lililouawa watu 12 Jumanne wiki hii.

Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kuwa wakazi wa mji huo na viunga vyake wamepigwa marufuku kutembea kuanzia saa 12:30 jioni hadi saa 12:30 asubuhi kwa kipindi cha miezi miwili.

Wakati huo huo mtu mmoja anayeshukiwa kuwa miongoni mwa walioendesha shambulizi hilo mjini Mandera amekamatwa.

Polisi inasema inamzuia Abdirahman Ali, aliyekamatwa katika nyumba ya wageni iliyoshmbuliwa mjini Mandera.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 anashukiwa kusaidia washambuliaji, kwa mujibu wa kikosi cha polisi cha Kenya kinachopambana dhidi ya ugaidi.

Shambulizi hilo lilidaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la Al Shabab.

Lakini jeshi lilikataa kuwa kundi la Al Shabab halihusiki moja kwa moja katika shambulizi hilo.