TANZANIA-KENYA-USHIRIKIANO

Rais John Pombe Magufuli ziarani Kenya

Jumatatu wiki hii Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, anafanya ziara ya kikazi katika nchi jirani ya Kenya. Na hii itakua ni ziara ya kwanza kwa kiongozi huyo tangu achukuwe hatamu ya uongozi wa nchi Alhamisi Novemba 5 mwaka 2015.

John Pombe Magufuli, Rais mpya wa Tanzania, Oktoba 30, 2015.
John Pombe Magufuli, Rais mpya wa Tanzania, Oktoba 30, 2015. REUTERS/Sadi Said
Matangazo ya kibiashara

Kuimarisha biashara kati ya Kenya na Tanzania ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa katika mkutano kati ya Rais John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta. Itafahamika kwamba Rais John Pombe Magufuli hakuweza kuhudhuria mikutano mikuu miwili iliyofanyika hivi karibuni katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Marais wengi kutoka Afrika walihudhuria mikutano hiyo.

Ziara ya Rais John Pombe Magufuli nchini Kenya, inakuja wakati ambapo uhusiano wa mataifa hayo mawili umekuwa ukilegalega.

Tangu kuchukua hatamu ya uongozi mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka jana, amezuru tu Rwanda na Uganda. Rais John Pombe Magufuli alionekana akisifiwa na Rais mwenzake wa Rwanda kutokana na kukabiliana na ufisadi nchini mwake, na ni rais ambaye anaongoza katika nchi nyingi za Afrika hasa ukanda wa afrika mashariki kwa kuvalia njuga ufisadi na rushwa huku akiweka mbele kazi, mslahi ya taifa na ya wananchi licha ya kukosolewa na baadhi ya asa wa upinzani.

Pia ziara ya Magufuli inahusina na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kumpendekeza Waziri wa mambo ya Nje wa Kenya Amina Mohammed kwa kinyanganyiro cha kuwania nafasi ya mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).