Habari RFI-Ki

Ziara ya Magufuli nchini Kenya kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ,biashara

Sauti 09:13
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (kushoto) akiwa na mgeni wake Rais wa Tanzania, John Magufuli (kulia), 30 October 2016
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (kushoto) akiwa na mgeni wake Rais wa Tanzania, John Magufuli (kulia), 30 October 2016 Kenya State House/ Media handouts

Rais wa Tanzania John Magufuli yupo nchini Kenya kwa ziara ya siku mbili, ya kwanza nchini humo tangu kuchaguliwa kwake .Rais Magufuli na rais Kenyatta wamezungumzia maswala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili. Rais Kenyatta na mwenyeji wake wamewahakikishia raia wa nchi hizo mbili kuwa, ni marafiki wa muda mrefu ambao utadumu. Maswala mengine yanayozunguziwa katika ziara hii mbali na biashara ni pamoja na ada inayotozwa kwa raia wa Kenya wanaofanya kazi nchini Tanzania, na maswala mengine ya ukanda ikiwemo hali ya kisiasa nchini Burundi na hali ya usalama nchini Sudan Kusini.