UGANDA-ELIMU

Chuo Kikuu cha Makerere chafungwa baada ya wiki 2 ya mgomo wa walimu

Baada ya wiki mbili ya mgomo wa wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Makerere kwa sababu ya kutolipwa fidia zao kwa miezi 8, Jumanne Novemba 1 vurugu zilizuka katika Chuo Kikuu hiki chenye wanafunzi karibu 40,000.

Chuo Kikuu cha Makerere mjini Kampala kikiwa chini ya ulinzi mkali Novemba 2, 2016.
Chuo Kikuu cha Makerere mjini Kampala kikiwa chini ya ulinzi mkali Novemba 2, 2016. RFI/Gaël Grilhot
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya wanafunzi walionesha kutoridhika kwao kwa kuchoma moto matairi, huku wakikabiliana na vikosi vya usalama ambavyo vilitumia mabomu ya machozi, mizinga ya maji kwa kuqatawanya waandamanaji. Baada ya makabiliano hayoe, rais wa Uganda alitangaza uamuzi wake Jumanne usiku wa kufunga Chuo Kikuu kwa muda usiojulikana (uvumi unasema kuwa Chuo Kikuu hiki kinaweza kufunguliwa baada ya Krismasi). Wanafunzi wanaoishikatika mabweni ya Chuo Kikuu walikua wamepewa muda wa kuondoa kabla ya jana Jumatano saa sita mchana. Zoezi hili lilifanyika kwa haraka na chini ya ulinzi mkali.

Wanafunzi wengi wanajutia kupoteza muda wao katika Chuo Kikuu cha Makerere kwa kipindi chote cha miaka mitatu, ambapo migomo ya mara kwa mara ilishuhudiwa, Baadhi ya wanafunzi wamesema kuelewa madai ya wahadhiri wao, lakini wanasema kusikitishwa na hatua ya kufunga Chuo Kikuu hicho. "Nina hasira kabisa, wewe unalipia masomo yako na kisha tunaambiwa ondokeni Chuo Kikuu kinafungwa, bila hata hivyo kujua kama tutarejeshewa fedha zetu. Huu ni mwaka wangu wa tatu na wa mwisho katika Chuo Kikuu. Hapakua matatizo katika miaka miwili ya kwanza lakini angali sasa kinachochotokea mwaka huu, " amesema Patricia, mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Makerere.

Baadhi wanasubiri ndugu zao wawatumie fedha ili waweze kurejea nyumbani kwa basi.

Hali ni shwari katika chuo Kikuu cha Makerere, polisi wanapiga doria kwa miguu na kwa gari. Kikosi cha kuzima fujo kimepiga kambi katika Chuo Kikuu hicho.